Main Title

source : Parstoday
Jumanne

14 Machi 2023

13:45:09
1352159

FBI: Uhalifu wa chuki dhidi ya wasio wazungu umeweka rekodi Marekani

Idara ya Upelelezi ya Marekani (FBI) imesema kuwa uhalifu wa chuki dhidi ya watu wa mbali tofauti uneongezeka kwa kasi nchini humo na kuweka rekodi ya juu zaidi.

Mojawapo ya madhihirisho muhimu ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Marekani, ambao umekuwa ukiendelea kwa mamia ya miaka katika nchi hiyo inayodai kulinda uhuru na haki za binadamu, ni ubaguzi wa rangi na mienendo ya kibaguzi dhidi ya watu weusi, kwa kadiri kwamba ubaguzi katika sekta ya elimu, kazi na ajira na katika masuala mengine mengi ya kijamii dhidi ya watu weusi umekuwa jambo la kawaida.

Ripoti iliyotolewa na Idara ya Upelelezi ya Marekani (FBI) imesema kwamba uhalifu wa chuki uliongezeka kwa takriban asilimia 32 mwaka wa 2021, na watu weusi ndio waliokuwa walengwa wa aina hizi za uhalifu.

FBI pia imetangaza kuwa 65% ya waathirika wa uhalifu wa chuki walilengwa kwa sababu ya rangi ya miili yao.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika visa zaidi ya 2,000, watu waliofanya uhalifu huu walifanya hivyo kwa nia ya kuwashambulia watu weusi.

Ripoti ya Idara ya Idara ya Upelelezi ya Marekani (FBI) inasema kuwa uhalifu wa chuki dhidi ya Wahispania na Waasia pia umeongezeka nchini humo.

Licha ya madai ya kutetea haki za binadamu na demokrasia huko Marekani, tabia na mienendo ya ubaguzi wa rangi katika nchi hiyo dhidi ya Waasia imeongezeka sana baada ya janga maambukizi ya Corona.

342/