Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

18 Machi 2023

18:25:03
1352915

Waziri wa Uingereza avitenga vyombo vya habari vinavyopinga mradi wa kupeleka wahamiaji nchini Rwanda

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza amevitenga na kuvibagua vyombo muhimu vya habari na kuvizuia kufuatana naye katika safari yake ya Rwanda ya kufuatilia mpango ulio dhidi ya wahajiri wa kuwahamisha wakimbizi katika nchi hiyo ya Kiafrika.

Gazeti la The Guardian, ambalo ni mojawapo ya vyombo vya habari vilivyobaguliwa na kuondolewa katika timu ya wanahabari ya Suella Braverman, limeandika katika ripoti yake kwamba, "gazeti hilo na mengine ya kiliberali, yamezuiwa kuwa katika safari hiyo iliyofadhiliwa kwa bajeti ya umma."

Ripoti hiyo inasema, kabla ya safari yake ya kwenda Rwanda siku ya Ijumaa, Suella Braverman alidai kwamba sera yake tata ya kuwafukuza wanaotafuta hifadhi nchini Uingereza na kuwapeleka Rwanda "itatumika kama kizuizi dhidi ya safari hatari na zisizo halali za wahamiaji."

342/