Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

18 Machi 2023

18:28:10
1352921

Morocco yasisitiza kuunga mkono kadhia ya Palestina

Serikali ya Morocco imetangaza kuwa, inaunga mkono na kuipa umuhimu kadhia ya Palestina na kwamba, inalitazama syuala hilo kama moja ya mambo muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu.

Hayo yameelezwa na Nasser Bourita, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Morocco ambaye amesisitiza kuwa, msimamo wa nchi yake wa kuunga mkono kadhia ya Palestina ni thabiti.

Akizungumza katika mkutano wa Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) huko Mauritania, Nasser Bourita amebnainisha kwamba, Morocco inatoa umuhimu mkubwa kwa kadhia ya Palestina na kwamba, hilo ni katika mambo yanayopewa kipaumbele katika sera za kigeni za taifa hilo.

Hata hivyo msimamo huo wa Morocco unakinzana na uhalisia wa mambo hasa baada ya nchi hiyo kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

Desemba 2020, Morocco na utawala haramu wa Israel zilifikia mapatano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida kwa ushawishi wa Marekani. Na kama sehemu ya makubaliano hayo, Rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump alikubali kutambua mamlaka ya Morocco juu ya Sahara Magharibi. Hata hivyo serikali ya rais wa sasa wa nchi hiyo Joe Biden imesema itauangalia upya uamuzi huo.

Mara kwa mara, wananchi wa Morocco wamekuwa wakifanya maandamano ya kupinga na kulaani hatua ya utawala wa kifalme wa nchi hiyo ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

342/