Main Title

source : Parstoday
Jumapili

19 Machi 2023

19:51:02
1353074

Muungano wa al Fatah: Marekani haitaki ISIS itokomezwe nchini Iraq

Mmoja wa viongozi wa Muungano wa al-Fath nchini Iraq ametangaza kuwa Marekani haitaki kuona kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) likiangamizwa kikamilifu nchini Iraq.

"Adi Abdul Hadi" amesema leo Jumapili kwamba, vyombo vya ujasusi vya Marekani ndivyo vilivyounda vikundi vya kimataifa vya itikadi kali, kama Al-Qaida na ISIS, na maelezo na kumbukumbua za baadhi ya wanasiasa wa Marekani vinathibitisha ukweli huu.

Abdul Hadi ameongeza kuwa, Marekani haitaki ISIS iangamizwe kabisa nchini Iraq, ndiyo maana inawahami na kuwalinda magaidi wenye uraia wa mataifa tofauti walioko katika kambi ya wakimbizi ya al-Hawl nchini Syria ili kuwatumia tena wakati mwafaka kwa ajili ya maslahi yake na kuyumbisha amani ya kanda ya Magharibi mwa Asia. 

Kiongozi huyo wa muungano wa al-Fath amesema Marekani inaliunga mkono kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) kwa njia tatu, moja ni msaada wa siri wa kifedha, ya pili ni kutoa taarifa muhimu kwa magaidi hao, na njia ya tatu ni kuwahamisha kutoka Syria na kuwapeleka Iraq.

Amesisitiza kuwa, Marekani haitaki kurejesha amani nchini Iraq na madai ya Washington kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi yapo kwenye karatasi tu na sio ya kweli.

Licha ya kushindwa kundi la kigaidi la Daesh nchini Iraq, idadi kadhaa ya wanachama wa kundi hilo bado wako katika maeneo tofauti ya Iraq na wanafanya vitendo vya kigaidi na mashambulizi ya kuvizia.

342/