Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

23 Machi 2023

12:40:21
1353595

Camarillo: Vijana hawana hamu ya kulitumikia jeshi

Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) ameeleza kuwa, ni vijana wachache sana nchini humo ambao wana hamu ya kufanya kazi jeshini.

Gabe Camarillo ameeleza kusikitishwa na kupungua ari ya vijana ya kulitumikia jeshi la Marekani na kwamba ni asilimia 9 tu ya kizazi cha vijana nchini humo ambao wameonyesha kuwa wapo tayari kuhudumu jeshini. 

Gabe Camarillo amesema, kiwango hicho cha vijana cha asilimia 9 waliotangaza kwamba wapo tayari kuhudumu jeshini ni cha chini kuwahi kuripotiwa huko Marekani katika muongo wa karibuni. Amesema, kizazi cha vijana wa Kimarekani hawajui lolote kuhusu suala la kuhudumu jeshini. 

Huko nyuma  pia, veterani mmoja Mmarekani alitabiri juu ya hatima ya kusikitisha itakayolikuma  jeshi la nchi hiyo iwapo  litalazimika kuingia vitani kukabiliana na vikosi vya ulinzi vya Russia. 

Wakati huo huo, Christopher Miller Kaimu Waziri wa Ulinzi  wa wakati wa utawala wa Rais Donald Trump hivi karibuni alibainisha katika kitabu chake cha kumbukumbu alichokipa jina la "Soldier secretary" kwamba: Jeshi la Marekani ni kubwa, lenye kutunisha misuli na kufuja bajeti, na kuandika kuwa: bajeti ya Pentagon inapasa kupunguzwa hadi nusu kwa sababu  jeshi la Marekani linapasa kubadilishwa na kuwa kikosi kidogo cha mapambano." 

342/