Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

24 Machi 2023

12:03:14
1353804

Kituo cha utafiti cha Bunge la Marekani: Machaguo yote ya kukabiliana na Iran yamegonga mwamba

Kituo cha Utafiti cha Bunge la Marekani kimekiri katika ripoti yake mpya kuwa, mikakati yote iliyotekelezwa na serikali mbalimbali za Marekani ili kuidhibiti Iran, ikiwa ni pamoja na "vikwazo vya kila upande, hatua za kiwango fulani za kijeshi, na mbinu za kidiplomasia" imefeli na kugonga mwamba.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Kituo cha Utafiti cha Kongresi ya Marekani kimekiri katika ripoti yake mpya iliyotumwa kwenye chombo hicho cha kutunga sheria cha nchi hiyo kwamba mikakati yote iliyotekelezwa na serikali mbalimbali za Marekani kwa ajili ya kukabiliana na Iran imeshindwa.Katika ripoti yake hiyo, kituo cha utafiti cha Bunge la Marekani kimeandika: "Kongresi imekuwa na nafasi kuu na muhimu katika kupanga sera za Marekani dhidi ya Iran; na katika muktadha wa vikwazo vipana kudhamini utoaji misaada na kutoa kibali cha kuuza silaha kwa washirika wanaotishiwa na Iran, kujaribu kujenga ushawishi katika mazungumzo yanayohusiana na mpango wa nyuklia wa Iran na kutunga sheria zinazohusu uchunguzaji wa makubaliano yanayofikiwa katika mazungumzo hayo". Katika sehemu nyingine ya ripoti yake hiyo, kituo cha utafiti cha Bunge la Marekani kimekiri kuwa sera tofauti za Marekani dhidi ya Iran hazijafanikiwa katika kuzuia ushawishi wa Iran na uwezo wa nchi hiyo wa kutoa changamoto kwa maslahi ya Marekani. Ripoti hiyo imeendelea kueleza kwamba: katika mwaka huu wa 2023, Iran ina ushawishi mkubwa katika eneo la Magharibi mwa Asia na inapanua mahusiano mapya na Russia na China; na kama ilivyokuwa hapo awali, ingali ina uwezo wa kutoa changamoto kwa maslahi ya Marekani katika eneo hilo na nje yake.../ 

 342/