Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

24 Machi 2023

12:04:17
1353806

Guterres atoa ujumbe kwa mnasaba wa kuanza Ramadhani, ahimiza kuweko dunia yenye haki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametuma salamu kwa Waislamu kote duniani akiwatakia kila la heri kwa mnasaba wa kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Katika ujumbe wake hhuo maalumu kwa mnasaba wa kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani, Antonio Guterres amesisitiza kwamba, Ramadhani ni mwezi wa "kutafakari na kujifunza.

Sambamba na kuwapongeza Waislamu kwa kkuwadia mfungo wa Ramadhani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa msukumo kutoka kwenye maadili ya mwezi huu uliobarikiwa ili kujenga ulimwengu wa haki na usawa kwa wote.

Ameongeza kuwa “Katika nyakati hizi ngumu, moyo wangu unajaa hisia za huruma na sala kwa ajili ya wale wanaopatwa na janga la migogoro, kulazimika kukimbia makwao na maumivu.  Naongeza sauti yangu kwa wale wote wanaoadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani, nikitoa wito wa amani, kuheshimiana na mshikamano.” 

Mapema mwezi huu, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliitisha mkutano wa ngazi ya juu kuadhimisha kwa mara ya kwanza siku ya kimataifa ya kupinga chuki dhidi ya Uislamu. Wakati wa maadhimisho hayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema kwenye ujumbe wake kwamba chuki dhidi ya Uislamu ni sumu.

Kadhjalika Guterres alisema, “Waislamu duniani ambao ni takriban bilioni mbili ni kielelezo cha ubinadamu katika utofauti wao na kubainisha kwamba wanatoka kila kona ya dunia, lakini mara nyingi wanakabiliwa na hali ya kutovumiliana na chuki bila ya sababu nyingine isipokuwa imani yao.”

Waislamu katika nchi nyingi za Kiislamu katika eneo la Asia Magharibu (Mashariki ya Kati), Afrika Mashariki na katika maeneo mengine ya dunia jana Alkhamisi walianza kutekeleza ibada ya Saum ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

342/