Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

25 Machi 2023

13:40:08
1354094

Umoja wa Mataifa watoa mwito wa kukabiliana na upungufu wa maji duniani

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuuwa, jamii ya kimataifa inahitaji kuchukua hatua sasa kukabiliana na upungufu wa maji safi.

Guterres, ameyasema hayo katika siku ya mwisho ya mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maji hapo jana uliofanyika kwa siku tatu katrika mji wa New York nchini Marekani.

Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, ni muhimu kuanzisha njia mpya za mifumo kupunguza matumizi ya maji yasiyo endelevu katika uzalishaji chakula na kilimo.

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti sasa hivi kuhakikisha rasilimali adhimu ya maji inalindwa, kudhibitiwa ipasavyo na kupatikana kwa kila mtu. 

Awali katika katika ujumbe wake kwa ufuunguzi wa mkutano huo, Guterres alikumbusha kuwa mabadiliko ya tabianchi yanaharibu mzunguko wa asili wa maji na uchafuzi wa gesi ya viwandani unaendelea kuongezeka hadi viwango vya kuvunja rekodi ya wakati wote huku ongezeko la joto duniani likifurutu ada kwa viwango vya hatari.

Mkutano huo umefanyika kwa mara ya kwanza baada ya karibu nusu muongo na kuibua matumaini ya kuchochea kasi ya kisiasa, katika kuimarisha hatua za kukabiliana na tatizo sugu la maji duniani.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, idadi ya watu wanaoishi mijini wanaotarajiwa kuwa kwenye mgogoro wa kukosa maji itaongezeka mara mbili kutoka watu milioni 930 mwaka 2016 hadi kufikia watu kati ya bilioni 1.7 na bilioni 2.4 mwaka 2050.

342/