Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

27 Machi 2023

11:29:05
1354505

Marekani yakiri kuwapa mafunzo wanaofanya mapinduzi ya kijeshi barani Afrika

Mkuu wa Kamandi Kuu ya Marekani Barani Afrika (AFRICOM) amekiri kuwa "maadili ya msingi" ya Pentagon yanayofundishwa kwa makumi ya maelfu ya maafisa wa kijeshi wa Kiafrika yanaendana na mapinduzi ya kijeshi.

Jenerali Michael Langley, mkuu wa majeshi ya Marekani ya AFRICOM, amesema: Kanali Mamady Doumbouya alihitimu programu ya mafunzo ya kijeshi ya Marekani, na Septemba 2021, ilipewa mafunzo ya "maadili ya msingi ya Pentagon" na hatimaye kuipindua serikali ya Guinea.

Matt Gaetz, mwakilishi wa chama cha Republican katika Bunge la Marekani, pia amenukuu makala ya Intercept na kufichua kwamba maafisa wa jeshi waliopewa mafunzo na Marekani wamefanya kwa uchache mapinduzi 8 yaliyofaulu katika Afrika Magharibi pekee tangu 2008.

Kabla ya hapo, Amadou Sanogo, afisa wa kijeshi wa Mali aliyefunzwa na Marekani, alikuwa ameipindua serikali ya nchi hiyo hapo mwaka 2012.

Sanogo alihusisha mafanikio yake na mafunzo ya kijeshi aliyopewa na Marekani na kusema: Nilijaribu kutumia kila kitu nilichojifunza Marekani hapa nchini Mali.

Kuwepo kwa majeshi ya Marekani katika nchi za Kiafrika kumezivuruga serikali za nchi za bara hilo na kuzidisha mivutano ya kisiasa na kijeshi.

342/