Main Title

source : Parstoday
Jumanne

4 Aprili 2023

13:18:36
1356138

Waingereza wabana matumizi kwa mbinu ya kula vyakula vilivyopita muda wa utumiaji

Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Uingereza imetangaza kuwa, watu katika nchi hiyo wanabana matumizi na kujiwekea akiba ya pesa kwa mbinu ya kutumia kiwango kidogo cha dawa na kula vyakula ambavyo muda wa matumizi yao umeshapita.

Kuanzia mwishoni mwa mwaka 2022, Uingereza imegeuka kuwa uwanja wa migomo ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali ikiwemo ya afya, usafiri wa reli na wafanyakazi wa posta kutokana na kutoridhishwa na ujira na mishahara wanayopewa na ongezeko kubwa la gharama za maisha.Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Uingereza imeripoti kuwa, robo ya vijana wanaotumia dawa walizoandikiwa na madaktari na kulazimika kujinunulia wenyewe, hutumia kiasi kidogo cha dawa hizo ili kupunguza gharama za matumizi ya fedha.Zaidi ya khumsi moja ya watu wote nchini Uingereza pia hutumia bidhaa ambazo muda wake wa matumizi umeisha kutokana na kuongezeka kwa mfumuko wa bei za vyakula.Mgomo wa wafanyakazi Uingereza

Takwimu hizo zinaonyesha matatizo ambayo familia nyingi nchini Uingereza zinakabiliana nayo kutokana na shinikizo ambalo halijawahi kushuhudiwa la viwango vya maisha na mishahara kutoendana na kasi ya upandaji bei.

Kulingana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Uingereza, 16% ya watu wazima wameainishwa kuwa ni tabaka lisilo na usalama wa chakula. Kutokuwa na usalama wa chakula kunamaanisha watu kutokuwa na uwezo wa kununua chakula cha kutosha ili kuishi maisha salama na ya afya.Watu ambao wana dalili za msongo wa mawazo huwa hawana shughuli za kiuchumi au hawana kazi au wanaishi katika maeneo ya watu wanyonge zaidi nchini Uingereza na wana uwezekano mkubwa wa kutokuwa na usalama wa chakula.../

342/