Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

7 Aprili 2023

14:48:51
1356632

Lavrov: Russia na Marekani sasa zimeingia kwenye awamu ya Vita Moto

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov amebainisha kuwa, nchi hiyo na Marekani sasa zimeingia katika awamu ya vita moto kutokana na muendelezo wa utumaji silaha kutoka nchi za Magharibi hususan Marekani kuelekea Ukraine kwa kisingizio cha vita katika nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la TASS, Lavrov ametangaza kwamba sababu nyingine inayoonyesha kuwa Moscow na Washington ziko katika awamu ya vita moto ni kwamba vikosi vya Ukraine vinapigana kwa kutumia zaidi silaha za Marekani, na serikali ya Marekani kila wakati inatishia kuipatia Ukraine mifumo hatari zaidi ya kuua na kuangamiza na yenye uwezo wa kufika masafa ya mbali zaidi kwa kisingizio cha vita katika nchi hiyo.

Sergei Ryabkov, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, naye pia amesema katika mahojiano aliyofanyiwa na shirika la habari la Sputnik jana Jumatano kwamba Russia na Marekani zimeshapita awamu ya Vita Baridi na kwa sasa ziko kwenye mapigano ya moja kwa moja.

 Hapo awali, Paul Craig Roberts, afisa wa zamani wa Ikulu ya White House wakati wa utawala wa Ronald Reagan, rais wa zamani wa Marekani alisema kuwa sera ya kutojali na kutochelea chochote ambayo inafuatwa na serikali ya nchi hiyo katika kuamiliana na Russia itasababisha mapigano ya nyuklia.../