Main Title

source : Parstoday
Jumapili

16 Aprili 2023

20:01:08
1358664

Rais wa Brazil aitaka Marekani iache kuchochea moto wa vita Ukraine

Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil amesema akiwa mjini Beijing, China kwamba Marekani inapaswa iepuke hatua za kuchochea moto wa vita nchini Ukraine.

Da Silva ameyasema hayo jana Jumamosi, katika siku ya mwisho ya ziara yake nchini China na kusisitiza kuwa: Marekani inapaswa iache kuhamasisha vita nchini Ukraine na badala yake ianzishe juhudi za kuleta amani.Aidha, Rais wa Brazil amesema: "Umoja wa Ulaya pia unapaswa kuanzisha juhudi za kutafuta suluhu na amani ili tuweze kuwashawishi Rais Vladimir Putin wa Russia na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine wakubali kwamba suluhu ni kwa manufaa ya kila mtu na kwamba kwa sasa vita vinavutia kwa watu hao wawili tu.Da Silva amefichua pia kwamba amejadiliana na mwenzake wa China Xi Jinping wazo la kuunda kikundi cha viongozi "wenye nia ya kutafuta njia za kuleta suluhu na amani."Kwa mujibu wa televisheni ya CNN, Rais wa Brazil amesema: "nina rai ambayo tayari nimeitetea katika mazungumzo na Emmanuel Macron (Rais wa Ufaransa), Olaf Schultz (Kansela wa Ujerumani) na Joe Biden (Rais wa Marekani) na tumeizungumzia kwa undani na Rais wa China.../

342/