Main Title

source : Parstoday
Jumapili

16 Aprili 2023

20:01:33
1358666

Katibu Mkuu wa UN ahimiza utiwaji saini mkataba wa kuzuia mauaji ya kimbari

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa nchi wanachama wa Umoja huo kujiunga na Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa mauaji ya Kimbari.

Bwana Guterres ametoa wito huo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa wakati wa tukio maalum la kumbukizi yam waka wa 29 tokea yajiri mauaji ya kimbari ya Rwanda, tukio lililofanyika kwenye ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu amesema pamoja na kujiunga na mkataba huo nchi wanachama lazima ziunge mkono ahadi zao kwa vitendo akisema kwa Pamoja hebu tuwe thabiti dhidi ya ongezeko la ukosefu wa stahmala. Hebu tuwe macho na tuwe tayari kuchukua hatua.

Mauaji hayo yalifanyika kwa siku 100 ambapo zaidi ya watu milioni moja, aghalabu wakiwa wa kabila Tutsi, wakiwemo Watoto, wanawake na wanaume waliuawa ambapo Katibu Mkuu amesema “tunaheshimu kumbukumbu ya waliopoteza maisha, wengi wao wakiwa Watutsi, lakini pia wahutu na wengineo waliopinga mauaji ya kimbari.”

Na zaidi ya yote ni kutoa heshima kwa manusura akisema tunatambua safari ya wanyarwanda kuelekea uponyaji, ujenzi mpya na maridhiano. 

Lakini kikubwa zaidi “tunakumbuka, tena kwa aibu, kushindwa kwa jamii ya kimataifa. Kushindwa kusikiliza – na kushindwa kuchukua hatua.

342/