Main Title

source : Parstoday
Jumapili

16 Aprili 2023

20:12:48
1358685

Wanajeshi 23 wa Marekani wameathirika ubongo kwa mashambulio ya maroketi nchini Syria

Baada ya muda kupita tangu vituo vya jeshi la Marekani viliposhambuliwa mashariki ya Syria, Kamandi Kuu ya jeshi la nchi hiyo (CENTCOM) imeripoti kuwa askari kadhaa wa jeshi hilo wameathirika ubongo kutokana na mashamulio hayo.

Mnamo Machi 24 mwaka huu vituo viwili vilivyowekwa kinyume cha sheria vya jeshi vamizi la Marekani katika maeneo mawili ya mafuta na gesi ya Konico na Al-Omar huko Deir Ezzor, Syria, vililengwa na mashambulizi ya maroketi.Duru za habari ziliripoti kuwa zaidi ya makombora 20 yalirushwa kulengwa kituo cha jeshi vamizi la Marekani katika eneo la visima vya mafuta la al-Omar nchini Syria.

Kwa mujibu wa Sky News, makao makuu ya Kamandi Kuu ya Marekani, ambayo kila mara hujaribu kuficha maafa yanayowapata askari wake wanaposhambuliwa katika eneo la Magharibi mwa Asia, ilitangaza katika taarifa kwamba wanajeshi 23 wa Marekani waliathirika ubongo kutokana na mashambulio yaliyofanywa dhidi ya vituo vyao katika mwezi uliopita wa Machi.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa timu za matibabu zinachunguza na kuangalia hali za wanajeshi hao wa Marekani ili kubaini athari hizo walizopata ni za aina gani.Inafaa kukumbusha kuwa katika mwezi wa Machi, wanajeshi wengine 25 Marekani walijeruhiwa na Mmarekani mmoja mstaafu aliuawa katika mashambulizi yaliyolenga wanajeshi wa Marekani nchini Syria.Ni mara kadhaa sasa ambapo Kamandi Kuu ya Marekani imeripoti mishtuko ya ubongo waliyopata wanajeshi wa Marekani wakati wa mashambulizi dhidi yao katika eneo hili.Mapema mwaka 2020, wanajeshi wapatao 100 wa Marekani waliathirika ubongo katika shambulio la makombora lililofanywa na Iran dhidi ya kituo cha anga cha jeshi la kigaidi la Marekani nchini Iraq.../


342/