Main Title

source : Parstoday
Jumatano

26 Aprili 2023

19:37:57
1360776

Russia Today: Ulaya imekuwa koloni la Marekani katika kadhia ya Ukraine

Chaneli ya televisheni ya Russia Today imeeleza katika ripoti yake ya uchambuzi kuhusu maandamano ya kupinga vita yaliyofanywa na watu kote barani Ulaya kwamba, Ulaya imekuwa koloni la Marekani katika kadhia ya Ukraine

Nchi za Magharibi na hasa Marekani zimezidisha mashinikizo ya vikwazo dhidi ya Shirikisho la Russia na kuipatia serikali ya Kiev kila aina ya silaha nyepesi na nzito, hatua ambayo si tu haijasaidia kuhitimisha vita vya Ukraine, bali imechochea na kukoleza zaidi moto wa mapigano katika nchi hiyo.Ugo Matti, mhadhiri wa chuo kikuu amesema katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Russia Today kwamba "tangu vilipoanza vita vya Ukraine, Italia ikiwa ni mwanachama wa shirika la kijeshi la NATO imetoa msaada wa kijeshi kwa Ukraine, lakini sidhani kama hatua hizi zina maslahi kwa Italia na NATO".Matti ameongeza kuwa, vita hivyo vinayanufaisha makampuni ya kutengeneza silaha tu nchini Marekani kama vile Lockheed Martin na kwamba wanaonufaika na vita hivyo ni makampuni yanayotengeneza silaha na zana za kivita.Mhadhiri huyo wa chuo kikuu nchini Italia amedokeza kuwa Marekani ina hamu kubwa ya kuendeleza vita; na kwa sababu ya maslahi hayo, jitihada zote zilizofanywa kwa ajili ya kuleta suluhu zimeyoyoma; wakati huo huo, Ulaya haipati manufaa yoyote, lakini kila inachokifanya ni kwa ajili ya maslahi ya makampuni ya utengenezaji silaha ya Marekani.Tangu vilipoanza vita vya Ukraine, hadi sasa Italia imepatia Ukraine vifurushi sita vya kijeshi. Vifurushi hivyo ni pamoja na yuro milioni 900 za msaada wa kijeshi. Aidha, serikali ya Rome imepanga kutoa mafunzo ya kijeshi kwa vikosi vya Ukraine.Hata hivyo, tangu mwaka jana, kumekuwa na maandamano mengi nchini Italia ya kupinga upelekaji silaha na zana za kijeshi nchini Ukraine. Mnamo mwezi Novemba, maelfu ya watu walimiminika kwenye barabara za mji mkuu wa Italia, Rome kutaka kukomeshwa upelekaji misaada ya kijeshi nchini Ukraine. Waandamanaji wallitangaza kuwa hatua hiyo inaathiri uchumi wa nchi yao.../

342/