Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

5 Mei 2023

18:03:10
1362923

Mafuriko DRC yaua watu 72, 40 hawajulikani waliko

Watu wasiopunua 72 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyotokea Alhamisi mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, eneo ambalo limekuwa likukumbwa na maafa kutokana na hujuma za wasi.

Wafanyakazi wa kutoa misaada wanasema mvua kubwa katika jimbo la Kivu kusini, imesbabisha mito kufurika na kupelekea hasara kubwa ya mali na vifo katika Kijiji cha Bushushu na Ntamukubi.

Mashirika ya kutoa misaada yanasema idadi kubwa ya waliofariki ni wanawake na Watoto. Aidha wakuu wa utawala katika mkoa huo wanasema  wamesema kwamba karibu watu 40 hawajulikani walipo.

Mafuriko na maporomoko ya ardhi hujiri mara kwa mara  katika jimbo la Kivu Kusini. Tukio la mwisho la kiwango kama hicho lilitokea Oktoba 2014, wakati mvua kubwa iliharibu zaidi ya nyumba 700. Zaidi ya watu 130 waliripotiwa kutoweka wakati huo.

Hayo yanajiri siku chache baada ya watu zaidi ya 130 kufariki dunia katika nchi jirani ya Rwanda kufuatia mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyoyakumba baadhi ya maeneo ya nchi hiyo

Nchini Uganda pia, ripoti zinasema vijiji kadhaa vilisombwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa ya hivi karibuni katika kanda hiyo huku watu wanane wakiripotiwa kuaga dunia.

Kwa mujibu wa shirika la Msalaba Mwekundu la Uganda wengi wa waliokufa ni wanawake na watoto.

Uganda kama ilivyo katika mataifa mengine ya Afrika Mashariki imekuwa na mvua kubwa. Meneja wa mawasilinao wa shirika la Msalaba Mwekundu Uganda amesema juhudi za kuwasaidia walioathirika zinaendelea.

Wakati huo huo, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema inafuatilia mifumo ya hali ya hewa kuhusu kunyesha kwa mvua za El Nino baada ya kuonesha kuwa mpaka sasa kuna uwezekano wa kunyesha mvua hizo kwa asilimia 60.

Hatua hiyo inatokana na taarifa ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) iliyoeleza kunyesha kwa mvua hizo nyingi katika nchi za Afrika Mashariki, Kusini mwa Afrika, Mashariki ya mbali na Amerika ya Kati.

Mvua hizo ambazo zimekuwa zikinyesha kila baada ya miaka miwili na kwa mara ya mwisho nchini zilinyesha mwaka 2016 na kusababisha madhara yakiwemo mafuriko.

342/