Janet Yellen amesema hayo mbele ya Kamati ya Fedha ya Kongresi ya Marekani na kueleza kuwa, vikwazo vya Washington vimepelekea nafasi ya sarafu ya dola katika miamala na mabadilishano ya kibiashara kuporomoka kwa kuwa aghalabu ya nchi zinafadhilisha kutumia sarafu nyingine na njia mbadala.
Waziri wa Fedha wa Marekani ameiambia kamati hiyo ya Kongresi kuwa, "Haistaajabishi kuona nchi zinazohofia kuathiriwa na vikwazo vyetu zinatafuta mbadala wa dola."
Duru za kiuchumi zinaarifu kuwa, wafanyabiashara wa mafuta duniani hivi karibuni wameanzisha kampeni ya kutumia sarafu mbadala, na kuachana na dola ya Marekani katika miamala yao.
342/