Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

16 Juni 2023

10:49:52
1373468

Uganda yajibu tahadhari ya Marekani, yasema: Hatutatishwa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda amesema taifa hilo kamwe halitasalimu amri na kukubali kuburuzwa na Marekani ili likengeuke thamani, maslahi na utamaduni wake.

Henry Okello Oryem amesema hayo akijibu onyo la serikali ya Washington la kuwataka raia wa Marekani wasisafiri kwenda Uganda, baada ya Kampala kupasisha sheria mpya dhidi ya ushoga inayochukuliwa kuwa moja ya sheria kali sana duniani ya kupambana na ufuska huo.

Waziri Oryem amesema katika mahojiano na gazeti la Monitor kwamba, "Marekani ina haki ya kutoa tahadhari ya usafiri kwa raia wao namna wanavyotaka, lakini vyovyote watakavyofanya sisi hatubabaishwi."

Waziri wa Mashauri wa Kigeni wa Uganda amesema taifa hilo la Afrika Mashariki halitakubali kuburuzwa na kushinikizwa kufanya jambo ambalo haliendani na thamani, utamaduni na maslahi ya Waganda.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni hivi karibuni pia alikataa wito wa nchi za Magharibi wa kufuta sheria hiyo dhidi ya ushoga iliyopasishwa na Bunge la nchi hiyo na kuidhinishwa na yeye mwenyewe mwezi uliopita.

Alisema, "Utiaji saini wa muswada wa kupinga ndoa za watu wenye jinsia moja umekamilika, hakuna mtu atakabadilisha hatua yetu. Tunapaswa kuwa tayari kwa mapambano."

Matamshi hayo ya Rais wa Uganda yalitolewa kujibu upinzani wa mashirika eti ya kutetea haki za binadamu na nchi za Magharibi zinazohamasisha ushoga na ndoa baina ya watu wenye jinsia moja. 

Serikali ya Rais Joe Biden wa Marekani imetishia kuwawekea vikwazo maafisa na viongozi wa serikali ya Uganda kwa sababu ya kupiga marufuku ubaradhuli na uchafu huo wa kimaadili. 

342/