Main Title

source : Parstoday
Jumanne

20 Juni 2023

08:44:55
1374179

Familia ya Biden yahusishwa na utakatishaji fedha katika kampuni ya gesi ya Ukraine

Barua pepe zilizofichuliwa na kampuni ya gesi ya Ukraine zinaonyesha kuwa Rais wa Marekani, Joe Biden na mwanawe walishiriki katika utakatishaji fedha wa kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa Daily Mail, Hunter Biden, mtoto wa Rais wa Marekani, Joe Biden na kampuni ya gesi ya Ukraine wameshiriki kuunda akaunti katika benki ya kigeni ambayo ilifungwa baada ya uchunguzi wa utakatishaji wa fedha chafu.

Barua pepe zilizopatikana zinaonyesha kuwa kampuni ya gesi ya Ukraine Burisma ilimwajiri mtoto wa rais wa sasa wa Marekani, Hunter Biden, mwaka 2014 na kuanzisha naye akaunti ya pamoja huko Malta, ambayo baadaye ilifungwa kufuatia uchunguzi wa uhalifu wa kifedha.

Kulingana na yaliyomo katika ripoti hizo zilizovuja, mmiliki wa kampuni ya Ukraine alituma dola milioni 10 kwa Hunter na baba yake, Joe Biden.

Mahakama ya Malta imetangaza habari kuhusu muamala wa kutiliwa shaka wa kampuni ya Burisma wa uuzaji wa mtambo wa kuzalisha mafuta.

Kufichuliwa uhalifu wa kifedha na ufisadi wa kimaadili wa mtoto wa Biden katika wiki za hivi karibuni, kumesababisha wimbi la ukosoaji dhidi ya Rais wa Marekani.

342/