Main Title

source : Parstoday
Jumapili

25 Juni 2023

19:53:22
1375345

Umoja wa Mataifa wataka kusitishwa mara moja 'mauaji ya kiholela' huko Darfur, Sudan

Umoja wa Mataifa umetaka kusitishwa haraka iwezekanavyo mauaji ya kiholela ya raia wanaokimbia mapigano huko Darfur magharibi mwa Sudan. Umoja wa Mataifa umesema kuwa maelfu ya miili ya watu ambayo haijazikwa imesalia mitaani na ndani ya nyumba katika jimbo hilo lililoathiriwa na vita.

Bi Ravina Shamdasani Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mtaifa amesema kuwa watu wanaokimbia mapigano huko El Geneina makao makuu ya jimbo la Darfur Magharibi wanapasa kudhaminiwa usalama katika harakati zao za kulikimbia jimbo hilo. Aidha amesema, mashirika ya misaada ya kibinadamu pia yanapasa kuruhusiwa kufika huko Darfur ili kukusanya miili ya watu waliouawa. 

Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ameeleza kusikitisha na mauaji ya kiholela katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan na kutilia mkazo kuchukuliwa hatua za haraka ili kukomesha mauaji hayo. 

Darfur, jimbo linalopatikana magharibi mwa Sudan katika mpaka na Chad mapema mwezi huu wa Juni lilikumbwa na machafuko na mapigano makali kati ya jeshi la Sudan na vikosi vya msaada wa haraka (RSF).  

Umoja wa Mataifa umegusia juu ya uwezekano wa kushuhudiwa jinai dhidi ya binadamu huko Darfur na kutahadharisha kuwa mzozo unaoendelea jimboni humo umechukua mwelekeo wa kikabila katika eneo hilo. 

342/