Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

1 Julai 2023

20:17:06
1376414

Mkuu wa CIA alifanya safari ya siri Ukraine kabla ya uasi wa Wagner

Magazeti ya Marekani yameripoti kuwa, Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) alifanya safari ya siri nchini Ukraine, siku chache kabla ya kufanyika uasi wa kundi la Wagner dhidi ya serikali ya Russia mnamo Juni 24.


Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post, William Burns, Mkurugenzi wa CIA alifanya safari ya kificho nchini Ukraine mwezi uliomalizika wa Juni, ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na majasusi wenzake pamoja na rais wa nchi hiyo, Volodymyr Zelensky.

Press TV imeripoti habari hiyo na kueleza kuwa, wakati wa mkutano huo, maafisa wa Ukraine walimwabia Burns kuhusu mpango wa Kiev wa kutwaa maeneo yanayoshikiliwa na Russia, na kuanzisha mazungumzo ya usitishaji vita kufikia mwishoni mwa wiki hii.

Afisa wa Marekani ambaye hakutaja jina lake amesema, Burns alienda Kiev kuihakikishia Ukraine kuwa Washington itaendelea kuipa taarifa za kijasusi ili eti iweze kupambana na uvamizi wa Russia.

Rais Vladimir Putin wa Russia alisema hivi karibuni kuwa aliagiza vikosi vya nchi hiyo vijiepushe na umwagaji damu wakati wa uasi wa kundi la Wagner mwishoni mwa wiki iliyopita, akisisitiza kuwa Ukraine na Wamagharibi walitaka kuona wananchi wa Russia wakiuana wenyewe kwa wenyewe.

Alisema uzalendo wa Warusi ulitoa pigo kwa maadui wa Russia, Wanazi mamboleo na Kiev, pamoja na walezi wao wa Magharibi, kwani walitaka kuona wanajeshi wa Russia wanamalizina wao kwa wao.