Main Title

source : Parstoday
Jumapili

2 Julai 2023

22:17:09
1376680

Chama kikuu cha upinzani Sierra Leone: Hatutashiriki uongozini

Chama kikuu cha upinzani nchini Sierra Leone kimesema kuwa hakitashiriki katika ngazi yoyote ya utawala nchini humo kuanzia Bunge hadi Mabaraza ya Serikali za Mitaa kufuatia kile kilichotajwa kuwa matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyogubikwa na "udanganyifu".


Rais Julius Maada Bio alichaguliwa tena kuiongoza Sierra Leone kwa muhula wa pili baada ya Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo Jumanne iliyopita kutangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa rais. Kwa mujibu wa tume hiyo, Julius Maada Bio alishinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 56.17 ya kura zilizopigwa. Chama kikuu cha upinzani na taasisi mbalimbali huko Sierra Leone zimepinag matokeo hayo. 

Wakati huo huo waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa walisema kuwa takwimu hazilandani na matokeo ya awali na ya mwisho ya uchaguzi wa Rais huko Sierra Leona na kusisitiza kuwa uchaguzi huo haukuwa na uwazi. Wamezitolea wito pande husika kufanya mazungumzo ya amani ili kutatua hitilafu zilizopo. 

Chama kikuu cha upinzani cha All People's Congress (APC) kinachoongozwa na Samura Kamara kimeshika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 41.16 ya kura zilkizopigwa kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Sierra Leone. Chama hicho kimesema hakitavumilia dhulma, ukandamizaji na unyakuzi wa mamlaka nchini Sierra Leone. 

342/