Ehsan Zohre Vandi, Mkurugenzi wa Turathi za Kiutamaduni
katika Idara Kuu ya Turathi za Kiutamaduni, Utalii na Sanaa za Mikono ya
Khrasan Razavi, amesema: Joshua Iguta Gatimu, balozi wa Jamhuri ya
Kenya hapa nchini Iran, leo ametembelea eneo la Bustani ya Makumbusho ya
Utamaduni na Historia ya Naderi mjini Mashhad.
Katika mahojiano na IRNA, Zohre Vandi ameongeza kuwa: katika ziara
hiyo, na baada ya kupatiwa maelezo ya sehemu ya historia za enzi za
Nader Shah Afshar na pia kujua sifa maalumu za kisanii za bustani
hiyo ya makumbusho, balozi wa Kenya na ujumbe aliofuatana nao wamevutiwa
na kusifia historia ya Naderi.
Kuhudhuria maonyesho ya sanaa za mikono ni sehemu nyingine ya
programu ya ziara ya balozi wa Kenya na ujumbe wake kwenye jumba la
kitamaduni na la kihistoria la Makumbusho ya Bagh-Nader, ambapo walipata
fursa ya kuelewa zaidi aina mbalimbali za bidhaa na sanaa za jadi za
Iran.
Balozi wa Kenya nchini Iran Joshua Gatimu
Jumba la kumbukumbu la kiutamaduni na kihistoria la Bagh-Naderi
Museum liko kwenye makutano ya barabara ya Mashahidi wa Mashhad umbali
wa mita 500 kutoka mahali ilipo haram tukufu ya Imam Reza AS.
Kaburi la Nader liko katika sehemu kuu ya Ibn Bagh ya makumbusho hiyo na kando ya kaburi hilo, kuna kumbi kuu mbili.
Moja ya kumbi hizo ni Jumba la Makumbusho la Silaha za Kale, ambapo
silaha za zama tofauti za historia ya Iran zinaonekana katika jumba
hilo la makumbusho.
Halikadhalika, picha za uchoraji zilizopambwa kwa taswira za Nader Shah
akiwa vitani na nyaraka za hati maridadi zilizoandikwa kwa mkono ikiwemo
historia ya safari za dunia za Naderi ni turathi zingine adhimu za
kihistoria zilizoko katika makumbusho hayo.
Ukumbi mwingine ni wa makumbusho ya athari, nyaraka na vifaa vya utawala wa Nader Shah.
Katika makumbusho hiyo kuna kaburi pia la Kanali Mohammad Taqi Khan Pesian, jemadari mzalendo wa Iran.../