Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

3 Julai 2023

20:48:21
1376916

Algeria yaiomba Misri iiruhusu Algiers iupe Ukanda wa Ghaza mafuta ya bure

Baadhi ya duru za habari za Kiarabu zimetangaza kuwa, Rais wa Algeria amemuomba rais mwenzake wa Misri kutoa kibali kwa Algeria kuupa mafuta ya bure Ukanda wa Ghaza.


Shirika la Habari la Kimataifa la Fars limezinukuu baadhi ya duru za habari za Kiarabu zikiripoti kwamba Rais wa Algeria, Abdel Majid Taboun amemwomba rais mwenzake wa Misri, Abdel Fattah Al-Sisi, kuruhusu serikali ya Algeria kuupitishia mafuta hayo ya bure katika ardhi ya Misri kueleka Ukanda wa Ghaza.

Gazeti la "Rai Elyoum" limeripoti kuwa, Rais Abdel Majed Taboun sasa anasubiri majibu ya Abdel Fattah al-Sisi ili aanze kupeleka shehena za mafuta ya bure kwa wakazi wa Ukanda wa Ghaza kupitia ardhi ya Misri.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Algiers imependekeza kudhaminiwa mahitaji yote ya mafuta na nishati ya Ukanda wa Ghaza kwa gharama ya hazina ya Algeria.

Duru za Algeria zimesema kuwa nchi hiyo inasubiri kupata jibu la moja kwa moja kutoka kwa serikali ya Misri kuhusu pendekezo hilo au kutajiwa sababu na vizuizi vya kushindwa kutekelezwa pendekezo hilo.