Main Title

source : Parstoday
Jumanne

4 Julai 2023

19:35:14
1377169

Papa akosoa vitendo vya kuvunjia heshima matukufu ya kidini

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amelaani kukaririwa vitendo vya kuvunjiwa heshima kitabu cha Waislamu cha Qur'ani Tukufu na kuvunjia heshima matukufu mengine ya kidini.

Katika mahojiano na gazeti moja la Umoja wa Falme za Kiarabu, Papa Francis amesema ameghadhabishwa na kukerwa na hatua ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu huko nchini Sweden.

Papa Francis ametilia mkazo suala la wafuasi wa dini mbalimbali kuishi pamoja kwa amani na maelewano, sanjari na kupinga misimamo na mitazamo ya kufurutu mipaka.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani amesema kuwa, uhuru wa maoni na kujieleza haipasi kuonekana kama idhini ya kitendo hicho cha fedheha cha kuvunjia heshima matukufu ya dini nyingine.

Papa Francis ameeleza bayana kuwa, kutumia 'uhuru wa maoni' kuonyesha dharau na chuki kwa wengine kunapasa kupingwa kwa nguvu zote na kulaaniwa vikali.

Waislamu kote duniani wamepaza sauti zao kulalamikia kitendo hicho kiovu cha kudhalilisha na kuvunjiwa heshima Qurani Tukufu nchini Sweden, huku kampeni kubwa ya dunia nzima ya kususia bidhaa zinazozalishwa na nchi hiyo ya Magharibi ikishika kasi.

342/