Main Title

source : ابنا
Jumanne

4 Julai 2023

20:24:51
1377171

Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia atahadharisha kuenea ghasia za Ufaransa katika nchi nyingine

Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia amesisitiza kuwa nchi za Ulaya zinapasa kubuni sera ili kuzuia machafuko yaliyoigubika Ufaransa kuenea katika nchi nyingine.

Antonio Tajani ametahadharisha kuhusu kuenea ghasia za Ufaransa huko Ubelgiji na Uswisi na kuongeza kuwa, maeneo yote yanayozungumza Kifaransa yamekumbwa na butwaa hivi sasa. "Tunapasa kutenganisha sababu zinazoibua machafuko na tuyapatie ufumbuzi matatizo kwa njia za kisiasa." 

Wimbi la hasira na ghadhabu za wananchi limeenea kote Ufaransa baada ya polisi wa nchi hiyo kumuua kwa kumpiga risasi Nahel Marzouq aliyekuwa na umri wa miaka 17 Jumanne iliyopita katika kitongoji cha  Nanterre huko Paris. Kufuatia kukasirishwa na na mauaji ya kijana huyo, wananchi huko Paris na katika maeneo mengine ya Ufaransa wamechoma moto magari na majengo mengi pamoja na kupelekea mamia miongoni mwao kutiwa mbaroni.  

Serikali imeimarisha ulinzi huku ikikata huduma za intaneti katika baadhi ya maeneo kufuatia maaandamano hayo makubwa ya wananchi. 

342/