Main Title

source : Parstoday
Jumatano

5 Julai 2023

17:57:46
1377417

Sakata: Cocaine ya Hunter Biden yapatikana ndani ya Ikulu ya Marekani

Ikulu ya White House ya Marekani imekumbwa na sakata jingine, baada ya kifurushi cha mihadarati aina ya cocaine kinachoripotiwa kuwa cha Hunter Biden, mtoto wa Rais wa Marekani, Joe Biden kupatikana ndani eneo la West Wing katika makazi hayo rasmi ya rais.

Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post, maafisa wa Kitengo cha Ulinzi wa Rais wa Marekani maarufu kama Secret Service (USSS), Jumapili iliyopita walipata kifurushi hicho na kudai kuwa ni kitu kisichojulikana.

Hata hivyo duru za habari zimeliambia gazeti hilo kuwa, kifurushi hicho kilikuwa cha mihadarati aina ya cocaine inayomilikiwa na Hunter Biden, mtoto wa kiume wa Rais wa Marekani ambaye anakabiliwa na kashfa nyingi za kimaadili na rushwa.

Chanzo kimoja ambacho kiko karibu na sakata hilo kimeiambia Idara ya Dharura na Zimamoto ya Washington kuwa, unga mweupe uliopatikana ndani eneo la West Wing katika Ikulu ya White House ni cocaine.

Haya yanajiri chini ya wiki mbili baada ya barua pepe zilizofichuliwa na kampuni ya gesi ya Ukraine kuonyesha kuwa, Rais wa Marekani, Joe Biden na mwanawe Hunter Biden walishiriki katika utakatishaji fedha wa kampuni hiyo. Kulingana na yaliyomo katika ripoti hizo zilizovuja, mmiliki wa kampuni ya Ukraine alituma dola milioni 10 kwa Hunter na baba yake, Joe Biden.

Aidha Juni mwaka jana, gazeti la Washington Examiner lilifichua kashfa ya ufuska inayoizunguka familia ya Rais Joe Biden wa Marekani, ambapo kiongozi huyo wa Marekani anaripotiwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kugharamia ufuska wa mtoto wake wa kiume, Hunter Biden.

Data zilizopatikana kwenye kipakatakilishi (laptop) cha Hunter Biden zilifichua kuwa, kijana huyo wa kiume wa Biden alitumia zaidi ya dola 30,000 kuwalipa makahaba wa Ulaya Mashariki, kati ya Novemba mwaka 2018 na Machi mwaka 2019, kipindi ambacho Joe Biden alikuwa Naibu wa Rais na Rais wa Marekani.

342/