Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

8 Julai 2023

20:21:28
1377982

Sasa Sweden yafikiria kupiga marufuku kisheria kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu

Sambamba na kuongezeka mashinikizo na maonyo ya kimataifa dhidi ya Stockholm baada ya kafiri mmoja kuivunjia heshima Qur’ani Tukufu mbele ya Msikiti mkuu wa mji huo, sasa Waziri wa Sheria wa Sweden amekiri hadharani madhara ya kiusalama ya kuvunjiwa heshima mambo matakatifu nchini humo na ametangaza kwamba sasa serikali ya nchi hiyo imeamua kuchunguza uwezekano wa kuharamisha na kupiga marufuku kuchomwa Qur'ani Tukufu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, baada ya raia mmoja wa Sweden mwenye asili ya Iraq kuchoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu mbele ya msikiti mmoja mjini Stockholm wiki iliyopita na kuzusha wimbi kubwa la hasira la mamilioni ya Waislamu kote uliwenguni, sasa serikali ya Stockholm inafikiria kuharamisha kuchomwa moto Qur’ani Tukufu na vitabu vingine vitakatifu nchini humo.

Kwa upande wake, shirika la habari la Sputnik limevinukuu vyombo vya habari vya Sweden vikitangaza kuwa, Gunnar Stromer, Waziri wa Sheria wa serikali ya nchi hiyo amesema: "Kuchomwa kwa Qur’ani katika siku za hivi karibuni (mjini Stockholm), kumeharibu usalama wa ndani wa Sweden.”

  Nalo gazeti la "ftonbladet la Sweden limeandika kuwa, Waziri wa Sheria wa nchi hiyo ametoa ufafanuzi zaidi akisema, kadhia ya hivi karibui zaidi ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu sasa imeilazimisha serikali ya Sweden kuchukua hatua; sheria ya kushughulikia kesi kama hizo inajadiliwa hivi sasa.

Amesema: Miongoni mwa mambo tunayoyachunguza ni namna ya kufanyia mabadiliko sheria [ambayo hadi sasa imekuwa ikitoa ruhusa ya kuchomwa moto Qur’ani Tukufu].

Ilikuwa ni siku ya Jumatano (Juni 28) ambapo Salwan Momika, raia wa Sweden mwenye umri wa miaka 37, alichoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu mbele ya Msikiti mkuu wa Stockholm, siku ambayo Waislamu Sweden walikuwa katika siku ya kwanza ya Idul Adh’ha. Mkimbizi huyo wa Iraq aliyepewa uraia wa Sweden alkivunjia heshima Kitabu kitakatifu cha Waislamu bilioni mbili kwa kibali cha mahakama ya Sweden na kwa ulinzi kamili wa jeshi la polisi la nchi hiyo ya Ulaya Magharibi.

Hasira za Waislamu kwa serikali ya Sweden hivi sasa ni kubwa kiasi kwamba serikali hiyo ya watu wenye chuki kubwa na Waislamu imeogopa na inaonekana inajipapatua pole pole ili kukwepa hasira za Waislamu.

342/