Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

8 Julai 2023

20:21:53
1377983

Marekani yafanya mazungumzo ya siri na Russia kuhusu kumaliza vita Ukraine

Kanali ya televisheni ya NBC News ya Marekani imenukuu baadhi ya duru zikisema kwamba,: Kundi la maafisa wa zamani wa usalama wa taifa wa Marekani wamekuwa wakifanya mazungumzo ya siri na maafisa wakuu wa Russia walioko karibu na Ikulu ya Kremlin.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, kundi la maafisa wa zamani wa usalama wa taifa wa Marekani wamefanya mazungumzo ya siri na kundi la watu mashuhuri wa Russia ambao wanaaminika kuwa wako karibu na Ikulu ya Kremlin.

Shirika hilo la habari limeinukuu televisheni ya NBC ya Marekani ikiripoti kwamba, maafisa hao wa zamani wa Marekani wamewahi kufanya mazungumzo pia na na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergei Lavrov. Madhumuni ya mazungumzo hayo ni kufungua kanali ya la mazungumzo juu ya namna ya kumaliza vita nchini Ukraine.

Maafisa wanne wa zamani wa Marekani na maafisa wawili wa hivi sasa sasa wa Russia wamesema kwamba mwezi wa Aprili, Sergey Lavrov alikutana na kundi hilo la maafisa wa Marekani kwa saa chache huko New York.

342/