Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

8 Julai 2023

20:27:11
1377995

Kutokana na hali mbaya ya uchumi, Uturuki yawatia mbaroni na kuwahamisha mamia ya wahamaji

Vikosi vya usalama nchini Uturuki vimewakamata mamia ya wahamiaji na kuwarejesha nchi walikotoka.

Uturuki inakabiliwa na hali mbaya ya uchumi, na kwa mtazamo wa wachambuzi wengi, kutimuliwa kwa wingi wahamiaji wanaoishi katika nchi hiyo kunachangiwa na suala hilo. Kila siku, vyombo vya habari vya Uturuki vinachapisha habari za kukamatwa au kufukuzwa watu waliokimbilia nchini humo kwa ajili ya kupata hifadhhi.  Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uturuki, vikosi vya usalama vimewagundua na kuwakamata wahamiaji haramu 697 katika mji wa Istanbul. Operesheni ya kuwanasa wahamiaji haramu inaendelea kufanywa katika kila pembe ya jiji hilo kwa kushirikisha timu za idara ya kupambana na usafirishaji wa wahamiaji kimagendo katika njia za mipakani, ofisi ya tawi la bandari ya baharini na idara za polisi. Wale wote waliokamatwa hadi sasa wamehamishiwa kituo cha kuwarejesha wahamiaji makwao. Wakati huo huo, Shirika la Habari la Anatolia limetangaza kuwa wahamiaji 197 tayari wamesharejeshwa katika nchi walizotoka. Katika upande mwingine, ofisi ya Jimbo la Kuja Ili nchini Uturuki imetangaza katika taarifa kwamba wahamiaji wote waliokabidhiwa kwa idara kuu ya uhamiaji ya jimbo hilo wamesharudishwa katika nchi zao baada ya kukamilisha taratibu za kiidara. Hata hivyo taarifa hiyo haijataja wahamiaji hao waliokamatwa au kufukuzwa nchini Uturuki wametokea nchi gani.../ 

342/