Main Title

source : Parstoday
Jumapili

9 Julai 2023

20:14:05
1378288

Human Rights Watch yakosoa ubaguzi dhidi ya Waislamu wa Kishia Bahrain

Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch limekosoa ubaguzi unaofanywa na utawala wa Bahrain dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo na kutoa mwito wa kuhitimisha ubaguzi huo.

Tamko hilo la Human Rights Watch limetolewa baada ya juzi Ijumaa vyombo vya usalama kuzuia kufanyika ibada ya Swala ya Ijumaa katika msikiti wa Imam Swadiq (as).

Taarifa ya Human Rights Watch sambamba na kukosoa mbinyo dhidi ya Waislamu wa Kishia nchini Bahrain imelaani ukandandazaji na kamatakamata inaofanywa na vyombo vya usalama dhidi ya wanaharakati wa Kishia.

Ripoti mbalimbali zinaonyesha, ubaguzi wa kidini na kimadhehebu na kubomolewa misikiti ya Waislamu wa Kishia ni miongoni mwa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu vinavyoshuhudiwa nchini Bahrain.

Jumuiya ya Kitaifa ya Kiislamu ya Al-Wifaq ya Bahrain imekuwa ikisisitiza kuwa, viongozi wa Bahrain wanatekeleza kwa makusudi siasa na sera za maudhi na manyanyaso ya kidini nchini humo na kwamba hatua kali hizo zimeshtadi baada ya vuguvugu la mapinduzi ya Februari 14, 2011.

Utawala wa Bahrain umekamata idadi kubwa ya raia wake ili kuzima maandamano ya wananchi dhidi yake. Licha ya hatua zote hio za utawala wa Aal-Khalifa, lakini harakati za mapinduzi ya wananchi zingali zinaendelea kwa ajili ya kutekelezwa matakwa yao halali na ya kisheria.

342/