Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

10 Julai 2023

16:10:59
1378523

IOM: Idadi ya wahajiri kutoka Afrika wanaokimbilia Yemen imeongezeka

Shirika la Kimataifa la Wahajiri (IOM) limetangaza kuwa takriban wahajiri 11,000 wa Kiafrika wameingia nchini Yemen katika muda wa mwezi mmoja.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Anatolia, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limetangaza katika ripoti kuwa: wahamiaji 10,800 wa Kiafrika waliingia nchini Yemen katika mwezi uliopita wa Juni. Kulingana na ripoti hiyo, watu hao hata hivyo wamepungua kwa asilimia sita kulinganisha na mwezi wa kabla yake, ambapo wahamiaji 11,463 walielekea nchini Yemen. Aidha, kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu wa 2023 hadi Juni 30, wahamiaji elfu 77, 130 walikuwa wameshaingia huko Yemen. 

Mnamo mwezi wa Mei, Shirika la Kimataifa la Wahajiri lilitangaza pia kuwa katika miezi minne ya kwanza ya mwaka 2023, wahajiri wapatao 40,000 wa Kiafrika waliwasili nchini Yemen.

 Yemen ni kimbilio la wahamiaji kutoka nchi za Pembe ya Afrika, hususan Ethiopia na Somalia. Wengi wa watu hao wanachukua hatua ya kufanya safari hizo hatari ili kuweza kufika katika nchi za Ghuba ya Uajemi, hususan Saudi Arabia.../

342/