Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

17 Julai 2023

16:36:52
1380056

Russia yawatahadharisha Wamagharibi kuhusu kutuma mabomu ya vishada huko Ukraine

Rais wa Russia amezitahadharisha nchi za Magharibi kuhusu kutuma mabomu ya vishada huko Ukraine kwa kisingizio cha vita. Rais Vladimir Putin amebainisha haya kufuatia uamuzi wa karibuni wa Marekani kuhusu kutuma silaha hizo zizilizopigwa marufuku kimataifa huko Ukraine.

Rais Vladimir Putin wa Russia jana Jumapili alijibu uamuzi huo wa Marekani kuhusu kutuma mabomu ya vishada huko Ukraine na kusema: Russia inaamini kuwa inayo haki ya kutoa jibu linaloshabihiana iwapo silaha hizo za vishada zitatumika dhidi ya nchi hiyo.  

Aidha Sergei Shoigu Waziri wa Ulinzi wa Russia aliwahi kusema kuwa kitendo cha Marekani cha kutuma Ukraine mabomu ya vishada kwa kisingizio cha vita nchini humo kinarefusha tu vita hivyo. Rais Joe Biden wa Marekani Ijumaa tarehe 7 Julai mwezi huu alithibitsiha katika mazungumzo na televisheni ya CNN kwamba Marekani imepasisha kuipatia jeshi la Ukraine mabomu ya vishada. Marekani imefanya hivyo katika kuendeleza hatua zake za kujitanua na kuiingilia vita huko Ukraine. Tangazo hilo la Marekani kutuma mabomu ya vishada nchini Ukraine limepingwa pakubwa na kukabiliwa na radiamali mbalimbali kimataifa. Kwani hata waitifaki wa Marekani ikiwemo Ujerumani, Uingereza, Canada na Uhispania pia zimetangaza waziwazi kwamba zinapinga uamuzi huo wa Washington. 

342/