Main Title

source : Parstoday
Jumatano

19 Julai 2023

15:35:58
1380591

Watu 34 wafariki dunia katika ajali ya barabarani nchini Algeria

Takriban watu 34 wamepoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotolewa alfajiri ya leo nchini Algeria.

Shirika la habari la Reuters limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, ajali hiyo imetokea baada ya basi la abiria kugongana na gari dogo katika jiji la Tamanrasset, yapata kilomita 1,500 kusini mwa Algiers, mji mkuu wa Algeria.

Idara ya zimamoto ya Algeria imesema katika taarifa kuwa, watu 34 wameaga dunia kwa kuteketea kutokana na moto uliozuka baada ya magari hayo kugongana. Watu 12 wameripotiwa kujeruhiwa kwenye ajali hiyo.

Habari zaidi zinasema kuwa, katika miezi ya hivi karibuni, nchi hiyo ya Kiarabu ya kaskazini mwa Afrika imeshuhudia ongezeko la ajali za barabarani.

Baadhi ya ripoti zinasema kwamba, sababu kuu iliyopelekea kushuhudiwa ongezeko la ajali za barabarani nchini humo ni madereva kuendesha magari kwa mwendo wa kasi.

Kwa mujibu wa polisi ya Algeria, watu zaidi ya 900 walipoteza maisha na wengine wengi walipata majeraha katika ajali zilizotokea nchini humo mwaka jana 2022.

342/