Main Title

source : Parstoday
Jumanne

25 Julai 2023

17:17:25
1382247

Venezuela yatetea malengo ya Palestina mkabala wa ubeberu wa Marekani

Muungano wa Chama cha Kisoshalisti cha Venezuela (PSUV) umekosoa kimya cha jamii ya kimataifa mkabala wa maangamizi ya kizazi yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina na kusisitiza msimamo wa serikali ya Caracas wa kutetea na kuunga mkono mapambano ya Palestina dehidi ya ubeberu wa Marekani.

Diosdado Cabello, Makamu wa Kwanza wa Mwenyekiti wa chama tawala cha Muungano cha Kisoshalisti cha Venezuela amesisitiza katika mazungumzo yake na ujumbe wa ngazi ya juu wa serikali ya Palestina kwamba: "Sisi ni wanajeshi wa mapambano ya Wapalestina na daima tuko tayari kuwaunga mkono wananchi wa Palestina."

Cabello pia amesisitiza  umuhimu wa kuchukuliwa hatua mataifa yote ambayo yameungana katika mapambano dhidi ya ubeberu, na kukosoa msimamo wa jamii ya kimataifa wa kunyamaza kimya mbele ya maangamizi ya kizazi yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wa Palestina. Makamu wa Kwanza wa Mwenyekiti wa chama tawala nchini Venezuela ameongeza kusema kuwa: "Dunia inafunga macho yake. Taasisi mbalimbali hazisemi ukweli, na dunia imekuwa kana kwamba hakuna kinachotukia." Katika mazungumzo hayo, Rawhi Fattouh Mkuu wa Baraza la Kitaifa la Palestina ambaye ameongoza ujumbe wa Palestina huko Caracas amesema: Watu wa taifa hilo sawa kabisa na wenzao wa Venezuela, ni wahanga wa mateso, ukandamizaji na propaganda za uwongo za ubeberu wa Marekani, utawala wa Kizayuni na waitifaki wao. Fattouh pia amesisitiza kuwa malengo ya Palestina ni ya amani na kwamba wananchi wa Palestina wana haki ya kupigania na kutetea ardhi yao ambayo imevamiwa na kughusubiwa kupitia vitendo vya mabavu na kupenda kujitanua vya utawala wa Israel. Tangu alipochukua madarakani rais wa zamani wa Venezuela, Hugo Chávez mwaka 1998, uhusiano kati ya Palestina na Venezuela uliimarika sana, na Rais wa sasa wa Venezuela Nicolás Maduro mwezi Januari 2009 alikata uhusiano wa kidiplomasia wa nchi hiyo na utawala wa Kizayuni wa Israel na wiki kadhaa baadaye Maduro alianzisha uhusiano wa kidiplomasia na Palestina.

342/