Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

29 Julai 2023

20:21:32
1383265

AU: Putin anataka kupatikane njia za kuhitimisha vita Ukraine

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) amesema kuwa, Rais wa Russia ameonyesha hamu ya kutaka kuhitimisha vita huko Ukraine.

Zaidi ya mwaka mmoja umepita sasa tangu kuanza vita kati ya Russia na Ukraine. Vita hivyo vilianza baada ya shirika la kijeshi la nchi za Magharibi, NATO kupuuza wasiwasi wa kiusalama wa Moscow na kwa lengo la kuipokonya silaha Kiev.  

Marekani na Ulaya zimeendelea kuchochea vita na mapigano huko Ukraine kwa kuipatia silaha na zana za kivita serikali yay Kiev sambamba na kuiwekea Russia vikwazo vya aina mbalimbali.  

Shirika la habari la Iran, IRNA limeripoti kuwa, Azali Assoumani Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) amesema akiwa katika mji wa Saint Petersburg nchini Russia kwamba: "Rais Vladimir Putin ametangaza kuwa yupo tayari kwa ajili ya mazungumzo na tunasubiri kuona Ukraine itakuwa na msimamo gani kuhusu suala hilo." Assoumani ameeleza kuwa Umoja wa Afrika unapongeza juhudi za Russia za kusaidia, kutoa mafunzo na kuimarisha uwezo wa rasilimali watu barani Afrika na kuongeza kuwa "wakati Russia inashinda, ni kana kwamba Afrika pia imeshinda." Kongamano la Pili la Uchumi na Masuala ya Kibinadamu la Russia na Afrika lilimalizika jana alasiri kwa kutolewa taarifa. Kongamano hilo lilitilia mkazo ulazima wa kufanyiwa marekebisho muundo wa Shirika la Biashara Duniani. Pande mbili za Afrika na Russia pia zimepasisha mpango wa ushirikiano kwa ajili ya mwaka 2023 hadi 2026. 

342/