Main Title

source : Parstoday
Jumapili

30 Julai 2023

15:06:03
1383597

Ousmane Sonko wa Senegal ashtakiwa kwa kuchochea uasi

Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko ameshtakiwa kwa kupanga uasi na makosa mengine mapya, kulingana na mwendesha mashtaka wa umma nchini humo.

Tangazo hilo linakuja wiki kadhaa baada ya Sonko kukutwa na hatia ya kueneza ufuska na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani hatua iliyozua ghasia kubwa kote nchini.

Sonko ambaye amekuwa akitumikia kifungo chake nyumbani Ijumaa aliitwa kusailiwa katika mahakama ya polisi katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.

Abdou Karim Diop, mwendesha mashtaka wa umma wa Senegal, amewaambia waandishi wa habari kwamba mashtaka mapya yanatokana na maoni aliyotoa Sonko na mikutano yake ya hadhara pamoja na matukio mengine tangu 2021, ikiwa ni pamoja na tukio la nyumbani kwake kabla ya kukamatwa kwake Ijumaa.

Mbali na kuchochea uasi, mashtaka mapya ni pamoja na kudhoofisha usalama wa serikali, vitendo vinavyolenga kuhatarisha usalama wa umma na kuibua machafuko makubwa ya kisiasa, kushirikiana na wahalifu na taasisi ya kigaidi na wizi.

Hakukuwa na maoni ya mara moja kutoka kwa timu ya wanasheria wa Sonko.Sonko alishika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa urais wa Senegal mwaka 2019 na anapendwa na vijana wa nchi hiyo. Wafuasi wake wanadai mashtaka dhidi yake ni sehemu ya juhudi za serikali za kumkosoa katika uchaguzi wa urais wa 2024.

Sonko amedai kuwa Rais Macky Sall ni dikteta huku wafuasi wa kiongozi huyo aliye madarakani wakisema mwanasiasa huyo wa upinzani amevuruga amani na utulivu nchini.

Sall mapema mwezi Julai alipunguza mvutano katika taifa hilo la Afrika Magharibi kwa kutangaza kuwa hatagombea muhula wa tatu wenye utata kufuatia miezi kadhaa ya sutafahumu na uvumi kuhusu nia yake.

Hivi karibuni Sonko, alionyesha ukaidi na kusema hataki maridhiano na Rais Sall na kuonya kwamba atavuruga uchaguzi mkuu mwakani iwapo atazuiwa kugombea kiti cha urais.

Katika mahijiano na televisheni ya France 24, alibainisha wazi kwamba, "Hakutakuwa na uchaguzi katika nchi hii, iwapo Rais Macky Sall atapinga kugombea kwangu."


342/