Main Title

source : Parstoday
Jumapili

30 Julai 2023

15:06:40
1383598

OIC yatoa wito wa kuachiliwa huru Rais wa Niger aliyepinduliwa

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetoa mwito wa kuachiliwa huru Muhammad Bazoum Rais wa Niger aliyepinduliwa.

Hussein Ibrahim Taha, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) sambamba na kuelezea wasiwasi alionmao kuhusiana na matukio ya Niger amebainisha kuwa, OIC inalaani vikali hatua na juhudi zozote zile za kuchukua madaraka kwa kutumia nguvu.

Katibu Mkuu huyo wa OIC mbali na kutoa mwito wa kuachiliwa huru Rais Bazoum ametaka pia kurejeshwa utawala wa katiba katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Kikosi cha ulinzi wa rais wa Niger siku ya Alkkhamisi kilimtia nguvuni Rais wa nchi hiyo, Mohamed Bazoum na kumuondoa madarakani. Kikosi hicho pia kimetangaza amri ya kutotoke nje. 

Televisheni ya taifa ya Niger ilitangaza juzi Ijumaa, kwamba kamanda wa kikosi cha ulinzi wa rais, Jenerali Abdourahmane Tchiani, ameteuliwa kuwa mkuu wa baraza la mpito la nchi hiyo.Tchiani alisema, katika hotuba yake kwenye televisheni ya taifa, kwamba wanajeshi walichukua mamlaka nchini Niger kutokana na hali ya usalama kuwa mbaya. Nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zimelaani hatua za kubadili kinyume cha sheria serikali huko Niger na kutoa wito wa kuachiwa huru haraka iwezekanavyo na bila ya masharti Rais wa nchi hiyo, Mohamed Bazoum na watu wake wa karibu. Tangazo hilo lilitolewa siku moja baada ya jeshi la Niger kutangaza kuwa limemuondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum.

342/