Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

5 Agosti 2023

19:06:18
1385017

Vikwazo vya Russia vyaongeza mno idadi ya watu wasio na nyumba mjini London Uingereza

Takwimu zilizotolewa na Kanali ya Upashaji Habari za Watu Wasio na Nyumba (CHAIN) zinaonesha kuwa, idadi ya watu waliopoteza makazi yao na wasio na nyumba za kudumu za kuishi katika mji mkuu wa Uingereza, London, imeongezeka kwa asilimia 10 ikilinganishwa na muda kama huo mwaka jana.

Vita vya Ukraine na vikwazo dhidi ya Russia zimetajwa kuwa ndizo sababu kuu za mfumuko mkubwa wa bei na kupanda vibaya gharama za maisha kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa huko Uingereza na nchi myingine nyingi za Ulaya.

Taarifa hiyo imesema pia kuwa, matokeo mabaya ya vikwazo vya Russia na vita vya Ukraine ndiyo sababu ya kupungua uwezo wa manunuzi wa watu katika nchi za Ulaya Magharibi kiasi kwamba baadhi ya kaya zinashindwa kujidhaminia hata mahitaji yao ya kimsingi kabisa. Takwimu za kanali ya CHAIN ambayo inajihusisha na habari za watu wasio na nyumba na wanaoishi barabarani zinaonesha kuwa, katika kipindi cha baina ya mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu, idadi ya watu wasio na nyumba za kuishi mjini London imeongezeka kwa asilimia 10 ikilinganishwa na muda kama huo mwaka jana 2022.

Takwimu hizo zinaonesha pia kuwa, karibu nusu ya watu waliopoteza nyumba zao za kuishi mjini London wamekumbwa na matatizo ya akili na wanahitaji uangalizi wa karibu wa madaktari.Baraza la Mji wa London limetahadharisha kuhusu kuongezeka idadi ya watu wasio na nyumba mjini humo na kukiri kwamba mgogoro huo haudhibitiki kutokana na gharama za juu za maisha na uchache wa nyumba za kuishi. Watafiti wamegundua kuwa, idadi ya watu wanaokimbilia kwenye nyumba za B&B za bei ya chini na zisizo na thamani ambazo zinatumiwa kuwekwa kwa muda watu wasio na nyumba, imeongezeka sana hivi sasa huko London, Uingereza. 

342/