Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

11 Agosti 2023

17:02:03
1386371

Magaidi wa Daesh washambulia basi la makuruta wa jeshi la Syria na kuua askari kadhaa

Basi lililokuwa limebeba makuruta wa jeshi la Syria limeshambuliwa na magaidi wakufurishaji wa Daesh (ISIS) katika mkoa wa Deir ez-Zur wa mashariki mwa nchi hiyo.

Genge hilo la kigaidi linaloungwa mkono na madola ya kibeberu ukiwemo utawala wa Kizayuni wa Israel limekuwa likishambulia vituo vya kijeshi vya Syria na kuua na kujeruhi watu katika mashambulio yao ya kuvizia. Jeshi la Syria nalo linaendeleza operesheni zake za kuisafisha nchi hiyo ya Kiarabu na mabaki ya magaidi wa ISIS. 

Televisheni ya Al Mayadeen imeripoti leo Ijumaa kwamba magaidi wa Daesh wamelivizia basi moja lililokuwa limebeba makuruta wa jeshi la Syria na kulishambulia katika eneo la jangwani la mkoa wa Deir ez-Zur. Hadi inaripotiwa habari hii, askari 20 wa Syria walikuwa wameuawa na wengine 10 kujeruhiwa.Basi hilo lilikuwa linawapeleka makuruta hao wa jeshi la Syria kwenye vituo vyao mbalimbali vya kazi katika mji wa Deir ez-Zur, lakini magaidi wa Daesh wamelivizia basi hilo jangwani na kuanza kulifyatulia risasi ovyo. Siku tatu zilizopita pia magaidi wakufurishaji wa Daesh walifanya shambulizi katika eneo la Ma'dan 'Atiq, mashariki mwa mkoa wa Raqqah dhidi ya basi la makuruta wa jeshi la Syria na kuua askari 10 na kujeruhi wengine kadhaa. Serikali ya Syria imefanikiwa mno kuyashinda magenge ya kigaidi yaliyomiminwa nchini humo kufanya mauaji dhidi ya maafisa wa serikali na wananchi wa kawaida ili kuisambatisha nchi hiyo ambayo ni nguzo muhimu katika kambi ya muqawama ya kupambana na utawala wa Kizayuni wa Israel. Maeneo mengi yaliyokuwa yametekwa na magenge hayo ya kigaidi na ukufurishaji yamekombolewa na serikali ya Syria kwa kushirikiana na waitifaki wake na hivi sasa operesheni za kuisafisha nchi hiyo na mabaki ya magaidi sambamba na kukomboa sehemu zilizobakia za ardhi ya nchi hiyo, zinaendelea.

342/