Kiwango cha uharibifu uliosababishwa na moto huo kilikuja kubainika zaidi siku nne baada ya kuusawazisha na kuufanya majivu mji huo wa kihistoria wa mapumziko, kuteketeza majengo na kuyeyusha magari. Kulingana na Shirika la Serikali Kuu ya Marekani la Usimamizi wa Masuala ya Dharura (FEMA) gharama za kuujenga upya mji wa Lahaina zinakadiriwa kufikia dola bilioni 5.5, huku zaidi ya majengo 2,200 yakiharibiwa au kuteketezwa na zaidi ya ekari 2,100 kuchomwa moto. Gavana wa Hawaii Josh Green ameeleza katika mkutano na waandishi wa habari kuwa idadi ya vifo itaendelea kuongezeka huku waathiriwa zaidi wakiendelea kupatikana.Idadi ya vifo vilivyotokana na moto huo uliozuka siku ya Jumanne iliyopita imelifanya tukio hilo kuwa janga baya zaidi la kimaumbile kukikumba kisiwa cha Hawaii, kuliko gharika ya tsunami iliyoua watu 61 mnamo 1960, mwaka mmoja baada ya kisiwa hicho kuwa jimbo la Marekani.
342/