Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

14 Agosti 2023

20:28:36
1387060

Rais wa Brazil amshauri Biden: Weka kando "mawazo yako ya kivita"

Rais wa Brazil amezindua kampeni mpya ya kuongeza gharama za ujenzi wa miundombinu na kuvutia wawekezaji kutoka nje, na amemshauuri Rais wa Marekani, Joe Biden, kuachana na mawazo ya kuchochea vita.

Tofauti na mtangulizu wake Jair Bolsonaro, Rais wa Brazil Lula da Silva, amejitenga na Marekani na hataki kuwa tegemezi kwa nchi hiyo kwa gharama yoyote, na anaamini suala la kuwa na uhusiano sawa na wa haki na nchi zingine ili kulinda maslahi ya watu wa Brazil.

Luiz Inacio Lula da Silva amesema katika hafla iliyofanyika Rio de Janeiro kwa ajili ya kupata uungaji mkono kwa mpango wa matumizi kwamba: "Tunamwambia Joe Biden kwamba kwa miaka mingi Merekani inafikiria tu juu ya vita na sio kuwekeza nchini Brazil. Jitahidi kutumia pesa kidogo kuwekeza katika nchi yetu kwa sababu kutaleta amani katika nchi hii."

Akizungumza na mawaziri wa serikali, magavana na wasimamizi wa biashara, Lula amesema viongozi wa Brazil wanapaswa kusafiri duniani "kuuza miradi hii."

Mipango ya Da Silva ni kusaidia kufadhili mpango wake wa "kuongeza kasi ya ustawi", unaojulikana kwa kifupi kwa jina la PAC.

342/