Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

14 Agosti 2023

20:29:07
1387061

Jeshi la Niger kumfungulia mashtaka rais aliyeondolewa madarakani

Jeshi la Niger linasema kuwa litamfungulia mashtaka rais aliyeondolewa madarakani, Mohamed Bazoum kwa tuhuma za kufanya uhaini.

Tangazo lililotolewa na jeshi la Niger limesema Bazoum na watu wa karibu yake watafunguliwa mashtaka kwa tuhuma za kufanya uhaini mkubwa na kudhoofisha usalama wa ndani na nje. 

Taarifa ya Jeshi la Niger imetolewa masaa machache baada ya viongozi wa Kiislamu kutoka Nigeria kuwasili nchini Niger ikiwa ni sehemu ya juhudi za kidiplomasia za kurejesha amani katika nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika ambapo taarifa zinasema wamepiga hatua katika upatanishi.

Kanali Meja Amadou Abdramane, mmoja wa wajumbe wa serikali ya Niamey, amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba "Serikali ya Niger imekusanya ushahidi wa kumfungulia mashtaka rais aliyeondolewa madarakani na washirika wake wa ndani na nje kwa uhaini mkubwa na kuhatarisha usalama wa ndani na nje wa Niger."Mohamed Bazoum, familia yake na washirika wake kadhaa wa karibu bado wanazuiliwa katika chumba cha chini cha makazi ya rais huko Niamey. Jumamosi Agosti 12, rais huyo aliyeondolewa madarakani wa Niger alitembelewa na daktari wake wa kibinafsi. Kulingana na daktari huyo, wote wanaozuiliwa "wanaendelea vyema" na Mohamed Bazoum "naye iko vizuri kiafya". Hata hivyo Bazoum mwenyewe amedai kuwa matibabu yaliyotengwa kwa ajili ya familia yake na yeye mwenyewe ni "ya kinyama na ya kikatili". Baada ya Burkina Faso na Mali, Niger inakuwa nchi ya tatu kujiondoa chini ya udhibiti wa Ufaransa na kupinga sera za mkoloni huyo wa Ulaya.

342/