Main Title

source : Parstoday
Jumapili

20 Agosti 2023

20:55:04
1388213

Wayemen wapinga kuwepo Wamarekani katika Bahari Nyekundu

Vyombo vya habari vya Yemen vimeripoti kuwa, upinzani wa wananchi wa kusini mwa nchi hiyo dhidi ya uwepo wanajeshi wa Marekani katika Bahari Nyekundu na kuingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo umeshika kasi zaidi.

Tovuti ya habari ya al-Mash'had al-Janoubi ya Yemen imeandika kuhusu uwepo wa wanajeshi wa Marekani katika Bahari Nyekundu kwamba: Katika kivuli cha matukio ya sasa katika maeneo ya kusini mwa Yemen na mashindano ya kimataifa ya kudhibiti utajiri wa eneo hilo, wasiwasi na ukosoaji wa wanasiasa na wanaharakati kusini mwa Yemen kuhusiana na kuwepo kwa wanajeshi wa Marekani katika eneo hilo unazidi kuongezeka.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, jeshi la Marekani linajaribu kujizatiti katika Bahari Nyekundu katika kalibu ya muungano wa kimataifa. Hii ni licha ya kwamba, harakati huru nchini Yemen zinakuona kuwepo wanajeshi hao kama uingiliaji kati katika masuala ya ndani ya Yemen.

Wanaharakati wa kisiasa wa kusini mwa Yemen wanaamini kuwa, uwepo wa vikosi vya jeshi la Marekani katika eneo hilo si kwa ajili ya kupambana na ugaidi, bali ni kwa shabaha ya kutimiza malengo ya kikoloni na kiuchumi, na kwamba njia za kistratijia za baharini na maliasili zenye thamani katika eneo hilo zinapaswa kudhibitiwa.

Ikumbukwe kuwa, maeneo ya kusini mwa Yemen kwa ujumla yanadhibitiwa na makundi ya waasi wanaotaka kujitenga wenye mafungamano na Saudi Arabia na Imarati. Vilevile wanajeshi wa Marekani na Uingereza wapo katika baadhi ya maeneo hayo.

342/