Ulyanov ameeleza katika ujumbe alioandika kwa muundo wa suali
kwenye mtandao wa kijamii "X" (Twitter ya zamani): tofauti gani kuu
iliyopo kati ya taasisi za Magharibi (Kundi la G7, NATO, Umoja wa Ulaya,
n.k) kwa upande mmoja na BRICS kwa upande mwingine?
Akaongezea kwa kusema: "Wanachama wote wa BRICS wana hadhi sawa. Je, unaweza kusema vivyo hivyo kuhusu taasisi za Magharibi?"
Katika mlinganisho unaofanana na huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia
Sergey Lavrov naye pia amesema, tofauti kati ya BRICS na G7 au miungano
mingine yenye mielekeo ya Magharibi ni kwamba wao wote wanaiangalia
Marekani.
Mwanadiplomasia mkuu wa Russia ameongezea kwa kusema: Viongozi wa
BRICS wanashughulikia masuala halisi, wakati wanasiasa wa Magharibi na
waandishi wao wa habari wanapendezwa zaidi na kutikisa ndimi zao.
Akizungumzia wanasiasa wa nchi za Magharibi na waandishi wao wa habari
walioizungumzia BRICS kwa dharau Lavrov amesema: "hii inaonesha kuwa
wanatikisa ndimi zao tu, wakati sisi tunatumia akili zetu na
kushughulikia masuala halisi."
BRICS ni jina la kundi la nchi zenye uchumi unaoichipukia na kukua. Jina
hili linatokana na herufi za kwanza za majina ya Kiingereza ya nchi
wanachama ambazo ni Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini.
Katika mkutano wa hivi majuzi, ambao uliandaliwa na Afrika Kusini na
uliofanyika katika mazingira ya makabiliano makali kati ya Russia na
China kwa upande mmoja mkabala na Marekani na Ulaya kwa upande mwingine,
maombi ya uanachama wa nchi sita yalikubaliwa. Ifikapo 2024, nchi sita
za Iran, Argentina, Ethiopia na nchi tatu za Kiarabu za Muungano wa
Falme za Kiarabu, Saudi Arabia na Misri zitaongezwa kwenye kundi
hilo.../
342/