Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

31 Agosti 2023

16:17:32
1390338

Makaburi mapya ya umati ya Wahindi Wekundu yagunduliwa nchini Canada

Makaburi ya umati ya Wahindi Wekundu, ambao ni wakaazi asili wa Canada, yangali yanaendelea kugunduliwa nchini humo.

Makaburi hayo mapya ya umati yamegunduliwa katika mji wa Saskatchewan jirani na shule moja ya bweni baada ya kufanya uchunguzi.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumepatikana makaburi ya umati ya watoto nchini Canada na hivyo kupelekea nchi hiyo kuendelea kukabiliwa na lawama za kimataifa. Watoto hao kutoka makabila asili ya Canada waliteganishwa na wazazi wao katika kipindi cha kuanzia mwaka 1890 hadi 1970 na kupelekwa katika shule za bweni ambazo zilikuwa zinasimamiwa na Kanisa Katoliki.

Baraza la William Lake First Nation katika eneo la British Columbia nchini Canada limewahji kutangaza kuwa, uchunguzi katika shule ya bweni ya Misheni ya St Joseph inayomilikiwa na Kanisa Katoliki umebaini kuwa kuna makaburi katika eneo la uwanja wa shule hiyo.

Shule hiyo ya bweni ya Kanisa Katoliki huko British Columbia ambayo ilifunguliwa 1891 na kufungwa 1981 ina historia chafu ya udhalilishaji wanafunzi ambao wote walikuwa wakaazi asilia Wahindi wa Canada. Wanafunzi wengi waliokuwa katika shule hiyo walilazimika kutoroka huku wengine wakijaribu kujiuzua na wengine wakifariki wakati wa kutoroka.

Kuanzia mwaka 1883 hadi 1996 zaidi ya watoto laki moja na nusu wa wakazi asilia wa Canada walilazimishwa kuishi katika shule makhsusi zilizokuwa zikisimamiwa na wamishonari na wahubiri wa Kikatoliki ili eti kuwaingiza katika jamii ya Canada.