Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

1 Septemba 2023

20:21:15
1390510

Umoja wa Mataifa wakosoa marufuku ya abaya shuleni Ufaransa

Msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu (OHCHR) amelaani uamuzi wa Ufaransa wa kuwapiga marufuku wanafunzi Waislamu kuvaa vazi la abaya.

Msemaji wa OHCHR Marta Hurtado alisema Jumatatu kwamba ingawa chombo cha Umoja wa Mataifa hakikuwa katika nafasi ya kutoa maoni kwa kina kutokana na kutokuwepo kwa taarifa juu ya uamuzi wa Ufaransa na mipango ya utekelezaji, "ni vyema kukumbuka kuwa kulingana na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu, vikwazo  kuhusu udhihirisho wa dini au imani, ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa mavazi, yaliruhusiwa tu katika hali ndogo sana - ikiwa ni pamoja na usalama wa umma, utulivu wa umma, na afya ya umma au maadili."

"Kwa kuongeza, chini ya sheria ya kimataifa ya haki za binadamu, hatua zilizopitishwa kwa jina la utulivu wa umma lazima ziwe sahihi, muhimu na zenye uwiano," aliongeza.

"Jambo jingine lilikuwa kwamba kufikia usawa wa kijinsia kulihitaji kuelewa vikwazo vilivyowazuia wanawake na wasichana kufanya uchaguzi huru, na kuunda mazingira ambayo yanaunga mkono maamuzi yao wenyewe, ikiwa ni pamoja na lakini sio tu katika uchaguzi wa mavazi."

Siku ya Jumapili, Waziri wa Elimu wa Ufaransa Gabriel Attal aliambia kituo cha TV cha TF1 kwamba kuvaa abaya hakutaruhusiwa tena shuleni.