Main Title

source : Parstoday
Jumapili

3 Septemba 2023

18:13:21
1390906

Kinara wa ghasia za uchaguzi wa 2020 nchini Marekani ahukumiwa kifungo cha miaka 18 jela

Jaji wa Marekani amemhukumu Ethan Nordean, kiongozi wa kundi lenye itikadi kali la mrengo wa kulia, Proud Boys, kifungo cha miaka 18 jela, kwa kuhusika katika shambulizi dhidi ya jengo la Kongresi, Capitol, mnamo Januari 6, 2021.

Mahakama ya Marekani imemtia hatiani Nordean kwa kula njama, lengo likiwa kuchochea vitendo vya uhalifu mwingine, na hukumu yake inahesabiwa kuwa kifungo kirefu zaidi katika kadhia ya shambulio dhidi ya Kongresi.

Mahakama hiyo pia imemhukumu Joseph Biggs ambaye alikuwa mmoja wa viongozi wakuu wa zamani wa kundi la Proud Boys, kifungu cha miaka 17 jela kwa kupatikana na hatia ya kuhusika katika shambulio la Januari 6 mwaka 2021 kwenye jengo la Bunge la Marekani.

Vyombo vya habari vya Marekani vimetangaza kuwa, Joseph Biggs, mwanajeshi wa zamani wa Jeshi la Marekani, alikuwa mmoja wa viongozi wa kundi la Proud Boys tawi la Florida.

The Proud Boys ilianzishwa mwaka wa 2016, na ni kundi la mrengo wa kulia linalomuunga mkono rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump. Kundi hilo linajumuisha wanachama wanaume pekee na linasema linaunga mkono haki za kumiliki bunduki na kutetea utamaduni wa Kimagharibi.

Mnamo Januari 6, 2021, mamia ya wafuasi wa Trump walisababisha fujo na vurugu kubwa katika jengo la Kongresi, wakati wabunge walipokuwa wakithibitisha ushindi wa mgombea wa chama cha Democratic, Joe Biden, katika uchaguzi wa rais uliofanyika Novemba 2020.Ghasia na machafuko hayo yalianza baada ya Trump - ambaye hakukubali kushindwa katika uchaguzi - kudai wkamba kura ya uchaguzi wa rais zimechakkachuliwa ili kumpendelea mpinzani wake, Joe Biden.

Watu watano waliuawa katika machafuko hayo na Bunge la Kongresi likakumbwa na shaghalabaghala kwa muda.

342/