Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, tovuti ya Kiukreni
ya Myrotvorets, ambayo huchapisha habari za kibinafsi za waandishi wa
habari na watu mashuhuri kutoka nchi tofauti za ulimwengu ili eti
kutambulisha maadui halisi wa nchi hiyo, imeorodhesha jina la kiongozi
wa Wakatoliki duniani, Papa Francis katika orodha yake nyeusi kwa sababu
ya matamshi yake yanayounga mkono historia na utamaduni wa Russia.
Ripoti hiyo imesema, tarehe 25 Agosti, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vijana, Papa aliwaambia vijana waliokusanyika huko St. Petersburg, nchini Russia, kwamba: Msisahau utambulisho wenu. Ninyi ni warithi wa Urusi Kubwa, watakatifu wa Urusi Kubwa, wafalme wa Urusi Kubwa, Peter the Great na Catherine II.
Akihutubia vijana hao wa Russia, Papa aliongeza kusema kuwa: "Ninyi ni warithi wa Urusi, songeni mbele na mjivunie mtindo wenu wa maisha na Urusi wenu, na muwe na furaha."
Matamshi haya ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani yameibua mijadala mingi katika nchi za Magharibi zinazoiunga mkono Ukraine na kwa msingi huo wananchi wa Ukraine wameliweka jina la Papa Francis katika orodha ya maadui wa nchi yao.
Miongoni mwa watu mashuhuri waliowekwa kwenye orodha nyeusi ya tovuti ya Kiukreni ya Myrotvorets ni pamoja na Henry Kissinger, waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Marekani, na Silvio Berlusconi, aliyekuwahi kuwa waziri mkuu wa Italia.
342/