Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

4 Septemba 2023

18:43:23
1391161

Corbyn akosoa uchochezi wa magazeti ya Wazayuni dhidi ya misikiti ya Uingereza

Kiongozi wa zamani wa chama cha Lebor nchini Uingereza amekosoa vikali ripoti inayopiga vita Uislamu ya gazeti la Kizayuni la Jewish Chronicle linalochapishwa mjini London na kutahadharisha kuhusu njama za kueneza chuki dhidi ya Waislamu zinazofanywa na vyombo vya habari.

Katika ujumbe wake aliotuma kwenye mtandao wa kijamii wa X, Jeremy Corbyn amepongeza shughuli zinazofanyika katika Msikiti wa Finsbury Park katika jimbo lake la uchaguzi na kusema, eneo hilo linaeneza amani, matumaini na mshikamano baina ya watu katika jamii.  

Jeremy Corbyn amesema hayo baada ya gazeti la kila wiki la Mayahudi la Jewish Chronicle kuchapisha ripoti ya uchochezi iliyoitaja hotuba ya raia wa Misri katika Msikiti wa Finsbury Park kuhusu ukombozi wa Quds tukufu kuwa ni "chuki dhidi ya Wayahudi". 

Mohammed Kozbar, katibu mkuu wa msikiti huo pia alimsifu Sheikh Ahmed Yassin, mwasisi wa harakati ya Hamas, ambaye aliuawa kwa maroketi ya Israel mwaka 2004, kuwa ni shahidi.

Sehemu nyingine ya ripoti ya Juish Chronicle imetoa madai dhidi ya misikiti mingine nchini Uingreza na kuendeleza kampeni ya kueneza chuki dhidi ya jamii ya Kiislamu, ikiishauri serikali ya London kufanya uchunguzi zaidi dhidi ya vituo vya Kiislamu.

Akijibu uchochezi huo, Jeremy Corbyn ameendeleza ujumbe wake kwenye mtandao wa X akisema: "Jamii yetu haitasambaratishwa na wale wanaotaka kueneza hofu kwenye vyombo vya habari."

Ikumbukwe kwamba muda si mrefu uliopita, jarida hilo la Kiyahudi la Jewish Chronicle lilichapisha mfululizo wa ripoti za uchochezi dhidi ya Kituo cha Kiislamu cha Uingereza na kutoa madai yasiyo na msingi ambayo yalipelekea kufungwa kwa muda kituo hicho.

342/